0
Diego Llorente ameondoka Real Madrid na kujiunga na Real Sociedad kwa mkataba wa miaka mitano.
Beki huyo alicheza misimu miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu za Rayo Vallecano na Malaga, ambako alikuwa akipata namba katika kikosi cha kwanza katika timu zote mbili .
Hiyo ni tofauti na ilivyokuwa ndani ya Santiago Bernabeu, ambako amecheza mechi mbili tu zote akitokea benchi tangu 2012.
Beki huyo mwenye miaka 23, alichezea Hispania katika mchezo wa kirafiki walioshinda 3-1 dhidi ya Bosnia-Herzegovina mwezi Mei mwaka jana, ni matumani yake kwa kuhamia La Real kuongeza nafasi yake ya kucheza timu ya taifa.
"Kila kitu nilichokisikia kuhusu San Sebastian ni kizuri," alisema. "Ninafuraha klabu kama Real Sociedad kuonyesha nia na kunisajili.
"Real Sociedad ni klabu yenye heshima kubwa ndani ya Hispania na Ulaya kwa ujumla."

Chapisha Maoni

 
Top