0
 Shirikisho la Soka Ufaransa (FFF) linatarajia kumtumia kocha Zinedine Zidane kuinoa timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali yanayokuja.
Mafanikio aliyopata Zidane ya kuipatia Real Madrid mataji mawili katika msimu wa 2016/07 ni jambo lililowashawishi uongozi wa FFF kutaka kumpa kikosi cha Taifa.
Nahodha huyo wa zamani wa Ufaransa, Zidane aliiwezesha timu yake ya Taifa kutwaa mataji ya Kombe la Dunia mwaka 1998 na Euro mwaka 2000.
Uongozi wa juu wa FFF bado unalifikiria jambo hilo, lakini wanampa kipaumbele kocha huyo wa Real Madrid.

Chapisha Maoni

 
Top