0
Mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata anatarajiwa kutua Manchester United wikiendi hii kwa ajili ya vipimo, huku timu hiyo ikitarajiwa kutangaza dau lake jipya la kumsajili.
Daily Mirror ilieleza kwamba dau la mchezaji huyo limefikia Pauni 65 milioni. Usajili wa mchezaji huyo unatajwa umelenga kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic ambaye anaondoka klabuni hapo.
Manchester United inatarajia kumtangaza mchezaji huyo hivi karibuni iwapo atafuzu vipimo vya kitabibu.
Mchezaji huyo amekuwa chaguo la kwanza la Jose Mourinho ili kupata mbadala wa Ibrahimovic.

Chapisha Maoni

 
Top