Shirikisho la Soka nchini TFF linatarajia kuitisha kamati Tendaji kujadili mambo mbalimbali ikiwemo sakata la kukamatwa kwa Viongozi wa juu wa Shirikisho hilo katika kesi ya Matumizi Mabaya ya Ofisi.
Akizungumza na Sports HQ ya EFM Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia amesema ni wajibu wao kukaa na kujadili namna ambavyo wanaweza kuendesha soka wakati Rais Jamal Malinzi na Katibu wake Mwesigwa Selestine wakiwa bado wanashikiliwa.
-Najua wajibu wangu kwa sasa, lazima tuitishe kikao cha kamati Tendaji ili tujue tunaendeshaje Soka katika kipindi hiki kigumu na tukikabiliwa na Uchaguzi, Sijajua ni lini Lakini ni muhimu kufanya hivyo" Karia Alizungumza.
Kesi.
Malinzi na Mwesigwa wapo Rumande baada ya kusomewa Mashtaka 28 yanahusiana na Matumizi mabaya ya Ofisi Tangu walipoingia Madarakani Mwaka 2013.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni