0

Klabu ya Soka ya Mtibwa Sugar imetangaza kuwasajili wachezaji wawili Mlinzi Hussein Idd akitokea JKT Oljoro na Mshambualiaji Salumu Ramadhan Kihimba aliyekuwa akiichezea Timu ya Polisi Morogoro.
Msemaji wa Klabu hiyo Thobias Kifaru Ligalambwike amesema wachezaji hao ambao ni damu Changa walionesha uwezo mkubwa na timu zao msimu uliopita hivyo wanaimani kabisa ya kuwa watawasaidia kufanya maajabu msimu ujao.
-Tumesajili Damu Changa kutoka JKT Oljoro na Polisi Morogoro na mbali na Hao tunategemea kuwapandisha wachezaji kama watano au Sita hivi kutoka Timu B" Kifaru Alisema.
Wawili Hao Wanatarajia kujiunga na Timu hiyo kwa ajili ya mchakamchaka wa msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania pamoja na mashindano mengine ikiwemo kombe la Azam Sports Federation.
Waliotemwa.
Aidha Klabu hiyo imeachana Rasmi na Nyota wao Sita wa kikosi cha kwanza ambao kwa Mujibu wa Kifaru ni kwamba Mikataba yao imemalizika na hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuongeza Mikataba yao.
-Kuna Baadhi ya Nyota wetu Mikataba yao imemalizika na hatutawatumia katika msimu unaokuja Hii yote ni Katika kutengeneza Kikosi Bora, na tunaamini kuwa wachezaji tutakaowasajili wataziba hayo mapengo" Kifaru Aliongeza.
Wachezaji hao ni Ally Lundenga, Ally Shomari aliyejiunga na Timu ya Simba SC, Salumu Kibaya, Mkongwe Vincent Barnabas, Maulid Gole pamoja na Said Bahanuzi.


Chapisha Maoni

 
Top