0

Wachezaji wa Barcelona, Xavi, Samuel Eto'o na Carles Puyol wametua Argentina tayari kushudia harusi ya Lionel Messi mchumba wake Antonella Roccuzzo.
Ndoa ya Messi inafungwa leo Ijumaa Juni 30, katika mji wake aliozaliwa Rosario, sherehe hiyo itafanyika City Centre Hotel na Casino.
Ndoa hiyo ya nyota huyo wa Argentina itaonyeshwa moja kwa moja kwa mashabiki wa Messi watakaokuwa nje katika TV kubwa, kwa mujibu wa AS.
Messi amewalika nyota 21 wa kikosi cha kwanza cha Barcelona cha sasa, pamoja na maswahiba wake katika safu ya ushambuliaji MSN, Neymar na Luis Suarez.
Wengine watakaokuwepo ni Sergio Busquets, Jordi Alba, Carles Puyol, Cesc Fabregas, Xavi na Samuel Eto'o.
Mke wa Sergio Aguero, Karina ataimba wimbo nyimbo ya kwanza katika sherehe hiyo.


Chapisha Maoni

 
Top