Kocha wa timu ya Taifa Stars, Salum Mayanga amesema kikosi chake kimestahili kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Cosafa nchini Afrika Kusini.
Stars ilipata nafasi hiyo baada ya kulazimisha sare 1-1 na Mauritius katika mchezo wake wa mwisho na kufikisha pointi tano sawa na Angola wakitofautiana kwa mabao.
Katika hatua hiyo ya robo fainali, Stars itakuwa na kibarua kigumu cha kupepetana na wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini 'Bafana Bafana’ siku ya Jumapili Juni 2.
“Tumepata tulichokuwa tunahitaji kwenye kila mchezo tuliocheza , haya ni mashindano ilibidi tucheze kwa tahadhari ndio maana hatukufunguka sana katika michezo yetu dhidi ya Angola na Mauritius.
“Hatukuwa na sababu ya kutufanya kuishia hatua ya makundi na kwa upande wa mchezo ujao tutaingia na plani yetu ambayo bila shaka itatusaidia katika mchezo huo.” alisema Mayanga
Hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo Tanzania inashiriki kama mwalikwa itaanza kutimua vumbi kesho Julai 1 kwa Botswana kucheza dhidi ya Zambia, Namibia wataumana na Lesotho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni