0

Uongozi wa Klabu ya Mbao Fc umefanikiwa kumbakisha Kwenye Timu kocha Mrundi Ndayiragije Etienne kwa msimu mwingine zaidi licha ya Vilabu mbalimbali Kuwa katika vita kali ya kuwania huduma yake.
Taarifa zinasema kwamba kocha huyo yupo Jijini Mwanza toka Jumatano iliyopita na tayari amemaliza mazungumzo na Viongozi wa Mbao na kwamba kwa mujibu wa ratiba alitakiwa kuanza kazi Leo Jumatatu wakati klabu hiyo ilipokuwa imeanza zoezi la kutafuta wachezaji wapya kwa njia ya Kliniki ya Mazoezi.
Mwenyekiti wa Klabu ya Mbao amethibitisha pasipo kuwa nashaka yoyote kuwa kocha huyo ni miongoni mwa Makocha ambao wataunda benchi la Ufundi kwa msimu ujao na kwamba kuanzia Jumanne ya Julai 4, ataanza kuonekana katika Viunga vya uwanja wa Sabasaba kuendesha Kliniki ya Wachezaji.
Ataanza Kuonekana.
-Kocha Etienne yupo na nadhani alikuwa na taratibu zake alizokuwa anazifanya ndio maana ameshindwa kuonekana leo, aliomba udhuru lakini ataendelea kuonekana kuanzia kesho na kuendelea” Njashi Alisema.
Alipoulizwa Muda wa Mkataba ambao Kocha huyo amesaini, Njashi alikuwa mzito kuweka wazi akisisitiza kuwa muda ukifika basi kila kitu watakiweka hadharani ikiwepo na kulitambulisha bechi nzima la Ufundi.
-Kuhusu mkataba hilo sitaliweka wazi kwa sasa, tutawaita waandishi wa habari kwa pamoja tutawatambulisha benchi zima la ufundi, hilo mtegee litakuwepo na tutatangaza vyote, kuwa na subira ni hivi karibuni” Alisema.
Alikuwa Lulu.
Kocha Ndayiragije amekuwa akiripotiwa kutamaniwa na Timu mbalimbali za Ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwemo Mbeya City, hata hivyo kulikuwa na Taarifa za kwamba Kocha huyo amejiunga na Simba SC ili akawe kocha Msaidizi kuziba nafasi ya Kocha Mganda Jackson Mayanja.


Chapisha Maoni

 
Top