Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Salum Shaban Mayanga amesema ameridhishwa na mazingira ya Kambi ya nchini Misri na anaimani watawajenga vyema kuelekea Mchezo wa kwanza Kundi L dhidi ya Lesotho kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika.
Mayanga amesema tangu walipofika wanaona wazi kuwa mazingira ya kambi ni mazuri na rafiki kabisa wa wachezaji wake kwani hakuna mchezaji anayelalamika, na ufanyaji wao mazoezi umekuwa mzuri.
-Mimi nikiri toka tumefika mazingira ya Kambi ni Mazuri na ni rafiki kwa Timu yetu kufanya mazoezi, wachezaji wetu toka tumefika wapo kwenye hali nzuri kiakili, kiafya na kiufundi kwani hatujapata matatizo yoyote, ni matumaini yetu kuwa kambi itatusaidia kufanya vizuri katika mchezo wetu dhidi ya Lesotho’ Mayanga alieleza.
Mchezo muhimu.
Mchezo Muhimu.Taifa Stars inayopiga kambi nchini Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Mchezo ambao umepangwa kuanza saa Mbili
usiku.
Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.
Chapisha Maoni