0
Kocha wa zamani wa Azam, Stewart Hall amebwaga manyanga katika klabu ya AFC Leopards ya Kenya baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya nchi hio.
Hatua hio imepelekea uongozi wa AFC Leopards kumkabidhi mikoba ya ukocha Dennis Kitambi aliyekuwa msaidizi wa Hall.
Kitambi ambaye ni kocha msaidizi wa zamani wa Azam ataiongoza AFC Leopards katika michuano ya Kombe la SportPesa. Mtihani wa kwanza wa Kitambi utakuwa dhidi ya Singida United katika mechi ya mtoano.
Hata hivyo tayari AFC Leopards imeshatamtangaza kocha Dorian Marin kuwa kocha mkuu wa klabu hio ambayo haikuwa na matokeoa mazuri katika ngwe ya kwanza.
Marin ataanza kazi baada ya michuano ya SportPesa kumalizika wakati Ligi Kuu Kenya ikiwa katika mapumziko.

Chapisha Maoni

 
Top