Uongozi wa Maafande wa Ruvu Shooting Jumatatu Hii wamekutana Kujadili Ripoti Ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzanzibar Malale Hamsini Keya Tayari kwa Maandalizi ya Msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Msemaji wa Klabu hiyo Masau Bwire ameuambia mtandao huu kuwa Mwenyekiti wa timu Kanali wa Jeshi na Mkuu wa Kikosi cha Jeshi (CO) 832 Ruvu JKT, Charles Mbuge, Ndiye anayeongoza kikao hicho cha kujadili ripoti hiyo ya msimu wa 2016/17.
Kusajili 6.
Masau amesema Katika taarifa ya Kocha Malale, pamoja na mambo mengine, ameshauri wachezaji 10 kuachwa na wengine 6 kutoka klabu mbalimbali kuongezwa ili kukiimarisha kikosi msimu mpya wa ligi 2017/18.
Msimu uliopita Ruvu Shooting walimaliza katika nafasi ya Sita wakiwa na Alama 36, ambazo ni Alama 4 juu ya Timu zilizoshuka daraja.
Chapisha Maoni