Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefanikiwa kufuzu hatua ya Robo fainali ya Kombe la COSAFA baada ya kutoka sare ya Bao 1-1 na Timu ya Taifa ya Mauritius katika Mchezo Mkali wa Kundi B uliopigwa katika uwanja wa Moruleng nchini Afrika Kusini.
Bao pekee la Taifa Stars katika mchezo huo lilipatikana katika kipindi cha pili dakika 69 baada ya kazi nzuri ya Simon Msuva ambaye alifunga bao la kusawazisha baada ya Mauritius kutangulia mapema dakika ya 67 kupitia kwa Perticots.
Tofauti ya Mabao.
Tanzania wanafuzu baada ya Mchezo mwingine wa Kundi hilo uliozikutanisha Timu za Angola na Malawi kumalizika kwa Sare ya 0-0 na hivyo Tanzania anapita kwa tofauti ya Mabao ya kufunga na Kufungwa licha ya Kuwa na alama Tano sawa na Angola.
Sasa Tanzania atakutana na Afrika Kusini katika hatua ya Robo fainali Jumapili ya Julai 2 katika Uwanja wa Royal Bafokeng uliopo katika Mji wa Bafokeng Nchini Afrika Kusini, ambapo kama atafanikiwa kupita atakutana na Mshindi wa mchezo kati ya Zambia na Botswana katika Nusu fainali.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni