Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepata watoto pacha wakati akiwa kwenye mechi ya Kombe la Mabara jana usiku Jumatano, huku Ureno ikitolewa kwa penalti 3-0 dhidi ya Chile.
Ureno iliondolewa kwa matuta baada ya kumaliza dakika 90 wakiwa hawajafungana katika mashindano hayo yanayoendelea nchini Urusi.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid aliondoka na huzuni uwanjani baada ya timu yake kutolewa. Hata hivyo muda mfupi alipata taarifa za kupata watoto pacha, jambo ambalo linaonekana atakosa mechi ya Jumapili kumpata mshindi wa tatu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni