Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli amesema kwamba zoezi la usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho hilo litaendelea Kama kilichopangwa Licha ya Baadhi yao kuwa katika matatizo.
Kuuli ameyasema hayo wakati Rais Jamal Malinzi ambaye alichukua fomu ya Kutetea Kiti chake akiwa ameshikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kwa tuhuma ya Matumizi Mabaya ya Ofisi.
Wakili Kuuli ameeleza kinagaubaga pasina tafuna Maneno kuwa zoezi litaendelea na hivyo kuanzia Juni 28 Wataanza zoezi la usaili kwa wagombea na kwamba atakayekosa atakuwa amejitoa Rasmi kwenye nafasi yake anayowania.
-Zoezi linaendelea na tunatarajia kuanza usaili Leo pamoja na kupokea mapingamizi mbalimbali zoezi hilo ni la siku Tatu, Hatutafanya mabadiliko yoyote kisa Baadhi ya wagombea wamepata matatizo, na utaratibu unajulikana wazi" Alieleza Kuuli.
Ni Kazi ya Serikali.
Kuuli Ameongeza kuwa wao kama Taasisi hawawezi kushangazwa na kile Kinachoendelea na hilo ni jambo la kawaida kabisa kwa vyombo vya Serikali kufanya kazi zao na kwa kuwa ni tuhuma Wanaamini wagombea wataendelea na zoezi hilo la uchaguzi.
-Serikali inaendelea kufanya kazi Zake kila Mara, tuhuma zinataratibu Zake hivyo wanaweza kuendelea na zoezi lililopo mbele yetu ikitokea Siku tatu zimepita bila kutokea sisi Tutakuwa Tumemaliza kazi yetu" Kuuli aliongeza.
Ikumbukwe kwamba TFF inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa Viongozi Agosti 12 mwaka huu Mjini Dodoma na hivyo Bado wanaendelea na michakato mbalimbali kuelekea siku ya Uchaguzi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni