Manchester United imelazimika kujitoa kwenye mbio za kumsajili Eric Dier baada ya klabu yake ya Tottenham kugoma kufanya mazungumzo ya kumuuza.
Awali, kocha Jose Mourinho alimuweka kwenye rada kiungo huyo Mwingereza ili kumsajili msimu huu wa kiangazi lakini mambo yameharibika.
Hivyo, baada ya kumkosa mchezaji huyo, Mourinho akili yake ameielekeza kwa nyota wa Chelsea, Nemanja Matic.
Manchester United ilianza kufanya mawasiliano na klabu ya Tottenham kuhusu mpango wake wa kumsajili Dier, lakini msimamo wa klabu hiyo ni kwamba mchezaji huyo haendi popote.
Chapisha Maoni