0
.Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe amefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Zawadi Msalla amesema Marehemu Linah Mwakyembe amefariki akipatiwa matibabu hospitali ya Agha Khan.
Anasema shughuli za msiba huo zinafanyika nyumbani kwa Waziri Mwakyembe, Kunduchi Beach jirani na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwananchi mtoto wa Marehemu George amethibitisha kifo cha mama yake huku akisema taarifa zaidi zitatolewa na baba yake.

Chapisha Maoni

 
Top