Manchester United imeshindilia mabao 5- 2 klabu ya La Galaxy ya Marekani katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jijini Los Anges kujiandaa na msimu huu.
Mshambuliaji Marcus Rashford alionyesha ubora wake mbele ya mshambuliaji mpya wa timu hiyo Romelu Lukaku baada ya kufunga mabao mawili.
Lukaku hakufanikiwa kupata bao kwenye mchezo huo jambo ambapo pia mashabiki walipata fursa ya kumuona dimbani kwa mara ya kwanza akiwa kwenye jezi ya Manchester United.
Mabao mengine yalifungwa na Merouane Fellaine, Henrikh Mkhitaryan na Anthony Martial.
Chapisha Maoni