0

Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' wamefungwa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Ukanda wa Afrika ya Kusini 'COSAFA' kwa Mabao 4-2 na Timu ya Taifa ya Zambia 'The Chipolopolo'.
Mchezo ulianza Kwa kasi na iliwachukua Tanzania dakika 14 kuandika bao kupitia kwa Mlinzi Erasto Nyoni kwa Njia ya Faulo iliyomshinda mlinda mlango wa Chipolopolo Allan Chibwe.
Bao hilo liliwaamsha Zambia na kuanza kucheza kwa juhudi kubwa kwa kupiga mipira mingi langoni mwa Tanzania Lakini Uimara wa Aishi Manula uliwanyima nafasi Zambia kuandika bao la Kusawazisha.
Aidha Tanzania walishindwa kuvumilia kasi ya Zambia ambapo dakika ya 43 ilipigwa Pasi ndefu ambayo ilimkuta Isaac Shamujompa aliyemwangalia Brian Mwila na kumpatia Mpira wa V-Pass ambaye Naye akamchambua Aisha Manula na kuandika bao la Kusawazisha.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya kabisa Tanzania Kwani dakika moja tu Kabla ya Mapumziko Uzembe Wa mabeki wa Tanzania ukawasaidia Zambia kupata bao la Pili kupitia kwa Justin Shonga.
Hadi Mapumziko Tanzania walikuwa nyuma ya Mabao 2-1 Huku tayari Kocha Mayanga akifanya mabadilko kwa kumtoa Erasto Nyoni aliyeumia na kumuingiza Raphael Daudi.
Kipindi cha Pili.
Tanzania walirudi kipindi cha pili wakiwa na hamu ya ushindi wakicheza kwa Nguvu na kushambulia kwa kasi Lakini hawakulinda Lango lao vyema, Kwani dakika ya 54 Zambia walifanya shambulizi La kushtukiza na katika harakati Gadiel Michael akanawa ndani ya 18 na mwamuzi Victor Gomes kutoka Afrika Kusini akaamuru penati iliyopigwa kiufundi na Jack Chirwa.
Baada ya kupata bao hilo Zambia walirudi kabisa langoni kwao na Kuzuia mashambulizi ya Taifa Stars na Mpira ulionekana kuwa upande wa Tanzania zaidi. Hata hivyo ile Hali ya kujisahau iliwagharimu Tena Tanzania Kwani Zambia walifanya shambulizi Hatari ambalo bila ajizi Abdi Banda akacheza madhambi na mwamuzi akaamuru Kupigwa Faulo Nje Kidogo ya 18 ambayo ilipigwa kiustadi na Justin Shonga na kuandika bao la Nne.
Bao hilo lilimrazimu kocha Shabani Mayanga kufanya mabadiliko kwa kumtoa Abdi Banda na kumuingiza Nurdin Chona na baadae Elias Maguli akatolewa na kuingizwa Thomas Ulimwengu.
Bao la Simon Msuva.
Mabadiliko hayo yalileta uhai eneo la Ulinzi na eneo la ushambuliaji hivyo kuwafanya Tanzania kuweka kambi eneo Zambia na Hatimaye babatiza babatiza ikamkuta Simon Msuva na kuwaandikia Tanzania bao la Pili katika dakika ya 83.
Hata hivyo bao hilo halikubadilisha chochote Kwani hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kutoka nchini Afrika Kusini Victor Gomez Tanzania 2 na Zambia 4.
Kipigo hicho kinawafanya Tanzania kuanza Maandalizi ya mchezo wa Kutafuta Mshindi wa Tatu Julai 7 Kati ya mshindwa wa mchezo mwingine wa Nusu fainali kati ya Zimbabwe na Lesotho.


Chapisha Maoni

 
Top