0
Dar Young Africans kwa mara ya tatu mfululizo wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano hayo baada ya kuwachapa Majimaji kwa mabao 2-1.
Licha ya Majimaji kuonesha mchezo mzuri katika mtanange huo ambao umefanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea, Yanga ndio ambao walionekana kuwa na uchu wa ushindi kuanzia dakika ya kwanza.
Yanga walipata bao la kwanza katika dakika ya 40 kupitia kwa Pius Buswita kwa goli safi la kichwa baada ya kupokea mpira kutoka kwa mlinzi wa pembeni Mwinyi Haji Mngwali.
Baada ya bao hilo Majimaji walionekana kucharuka na kutaka kupata bao la kusawazisha lakini hali ikawa mbaya zaidi baada ya Emmanuel Martin kufunga bao la pili baada ya kupokea pasi kutoka kwa Hassan Kessy kushoto mwa lango la Majimaji.
Bao pekee na la kufutia machozi la Majimaji katika mchezo huo limefungwa na Jaffary Mohamed katika dakika ya 61 kwa kichwa safi kilichomshinda kipa Mkameruni Youthe Rostand.
Vikosi vilivyocheza.
Majimaji FC: Salehe Malande, Aziz Sibo, Mpoki Mwakinyuke, Juma Salamba, Idrisa Mohamed, Hasan Hamis, Lucas Kikoti, Yakubu Kibiga, Marcel Kaheza, Peter Mapunda na Jafar Mohamed
Akiba : Hasheem Mussa, Poul Lyungu, Geofrey Mlawa, Jerryson Tegete, Ramadhan Kapera, Sunday Leonard na Abubakar Halifa.
Yanga SC: Youthe Rostand, Hassan Kessy, Mwinyi Haji Mngwali, Said Juma, Kelvin Yondan, Pato Ngonyani, Emmanuel Martin, Papy Kabamba, Pius Buswita,Raphael Daud na Ibrahim Ajib.
Akiba: Ramadhan Kabwili, Juma Abdul, Makka Edward, Yussuf Mhilu Baruhan Yahya, Said Mussa na Geoffrey Mwashiuya.
Buseresere 0-3 Mtibwa
Aidha katika mchezo ulioanza mapema saa nane mchana, kati ya mabingwa wa mkoa wa Geita Buseresere FC na Mtibwa Sugar, umeshuhudia wakata miwa wa Turiani wakikata tiketi ya kucheza robo fainali baada ya kuwachapa wenyeji wao kwa mabao 3-0.
Mabao ya Mtibwa Sugar katika mchezo huo ambao umepigwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, yamefungwa na Hassan Dilunga, Haruna Chanongo na Ally Makarani.
Aidha ushindi huo kwa Mtibwa umerejesha kumbukumbu mbaya waliyoipata mwaka 2004 baada ya kufungiwa na shirikisho la soka Afrika (CAF) kushiriki michuano mitatu ya kimataifa kama wakifanikiwa kufuzu.
Ikicheza kwa mara ya kwanza michuano ya Caf mwaka 2004 Mtibwa Sugar ilifanya ‘kituko’ cha aina yake baada ya kutopeleka timu jijini Cape Town kwa ajili ya mchezo wa marejeano dhidi ya Santos FC. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika hapa nyumbani Mtibwa ilichapwa 3-0 na hivyo walihitaji ushindi unaoanzia magoli manne ugenini.
Kitendo hicho kiliwafanya wafungiwe na Caf miaka isiyopungua mitatu kucheza michuano yoyote ya Shirikisho hilo la soka Afrika.

Matokeo mengine hatua ya 16 bora
Njombe Mji 1-1 Mbao FC (Pen 6-5)
KMC 1-3 Azam FC
Singida United 2-0 Polisi Tanzania
Mechi zinazofuata
25 February 2018
19:00 JKT Tanzania vs Ndanda FC
26 February 2018
14:00 Kiluvya United vs Tanzania Prisons
16:00 Stand United vs Dodoma FC

Chapisha Maoni

 
Top