0
Mshambuliaji wa zamani wa England Wayne alifunga bao lake la kwanza katika klabu ya DC United na kupata jeraha la pua katika ushindi wa nyumbani wa 2-1 dhidi ya Colorado Rapids katika ligi ya MSL.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, alifunga bao la ufunguzi baada ya kupokea mpira kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Tim Howard.
Kellyn Acosta alifunga bao la kusawazisha kabla Howard kumnyima mara mbili nahodha wa DC Rooney.
Bao la pili la Niki Jackson lililofungwa mnamo dakika ya 90 liliipatia DC United ushindi kabla ya Rooney kupata jeraha la pua alipokuwa akiuzuia mpira.
Baadaye aliandika kwenye ukurasa wake waTwiter kwamba 'anajivunia kufunga bao lake la kwanza kwa DC United', akiongeza kwamba 'amepata jeraha la pua na ameshonwa mara tano'
Meneja wa DD United Ben Olsen amempongeza mshambuliaji kwa kuanza mechi kwa kishindo baada ya kuondoka Everton mwezi uliopita
''Kwa fikra zangu sidhani kwamba ni mara ya kwanza amejiunga na ameweza kuumudu vizuri mchezo. Ni mkakamavu na nadhani ataweza kuitisha timu yetu, Olsen amesema.
Amekuwa mchezaji wa kuvutia sana katika kila nyaja. Kama tulivyomtaka katika kikosi hiki- na kwa uongozi wake na uwezo wa kuyafunga magoli . tunamatumaini, mambo yataendelea kuwa kuwa bora zaidi.



Kwamujibu wa
BBC 

Chapisha Maoni

 
Top