Kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte amepata zali baada ya kutengewa Pauni 5.5 milioni kwa mwaka kuinoa AC Milan.
Kocha huyo amekaa nyumbani takribani wiki tatu tu tangu atupiwe virago vyake Stamford Bridge kutokana na matokeo mabaya ya Chelsea katika Ligi Kuu msimu uliopita.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Express, AC Milan wameamua kumpa ofa hiyo nzito Conte ili achukue nafasi ya Gennaro Gattuso wakiamini anao uzoefu wa kutosha kuipa makali timu hususani kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Conte alitimuliwa na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kwa kashfa licha ya kwamba msimu mmoja kabla alipongezwa kwa kuipa Chelsea ubingwa wa Ligi Kuu England na Kombe la FA.
Chelsea baadaye ilimuajiri Mtaliano mwenzake Maurizio Sarri, aliyetoka kuipa mafanikio Juventus pia ya Italia.
Chapisha Maoni