KIUNGO wa kimataifa wa Croatia, Luka Modric ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa kiume wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa taji la tatu la Ligi ya Mabingwa.
Hiyo ni baada ya kuwapiku washambuliaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah na w Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia.
Ronaldo ameshinda tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Msimu uliopita akiwa na Real Madrid baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mara ya sita, wakati Sergio Ramos ameshinda tuzo ya Beki Bora na Modric amechukua pia tuzo ya Kiungo Bora.
Kipa wa Real na Costa Rica, Keylor Navas ameshinda tuzo ya nne na ya mwisho usiku huu, baqada ya kutangazwa ndiye ya Mlinda Mlango Bora wa Msimu baada ya kuipa timu yake taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Penille Harder wa Wolfsburg ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Kike wa UEFA.
Nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, David Beckham ameshinda tuzo ya Rais wa UEFA baada ya kazi nzuri yake nzuri anayoendelea kuifanya kwa mchezo huo japo amestaafu.
Chapisha Maoni