Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk ya Belgium na mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan Thomas Ulimwengu wametua nchini tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo inayojiandaa kuivaa Uganda wikiendi hii jijini Kampala.
Stars inajiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Uganda, mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka wa Tanzania na Uganda.
Wachezaji wengine wanaokipiga nje ya Tanzania ambao wamejiunga na kambi hiyo ni pamoja na Rashid Mandawa anayekipiga nchini Botswana na Ramadhani Kessy anayetokea nchini Zambia.
Chapisha Maoni