![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhz75qIo_DuDPEQSQIdDDyqsEqpwyFm8lH60FJ6l6QRrWsf0PmcDvgbh-Q_yptldhFVyUWPT2OK6GWlTcDNNuR6__ho2hdGyy5YXYK0uxj0ZlASDykfYjQcU31yxEuTKbAVCMB5pm6aWR36/s640/1_5.jpg)
mkoani Dodoma limetupiliwa mbali katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Pingamizi hilo lilikuwa la kupinga ombi
lililowasilishwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) waliofungua kesi ya kikatiba
wakiomba mahakama itoe zuio la kuendelea kwa vikao vya Bunge maalumu la katiba hadi kesi hiyo
itakapokwisha.
Aidha, wanaomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) awasilishe bungeni muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba namba 8 ya mwaka 2011 na namba 2 ya mwaka
2012, sura ya 83 na ifafanue kifungu cha 25 cha sheria hiyo.
Uamuzi huo ulitolewa jana na jopo la majaji watatu wanaosikiliza ombi hilo wakiongozwa na Jaji Augustine Mwarija, Dk Fauz Twaib na Aloyisius Mujulizi.
Wakati huo huo, kesi nyingine ya kikatiba iliyofunguliwa na Mwandishi wa Habari, Saidi Kubenea akihoji mamlaka ya Bunge hilo inaanza kusikilizwa leo ambapo ilitakiwa ianze kusikilizwa
jana lakini AG aliwasilisha pingamizi ambalo pia litaendelea kusikilizwa leo.
Katika kesi hiyo, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba, kwa kuzingatia kifungu cha 25 (1) na (2)
cha Sheria ya Mbadiliko ya Katiba namba 83 ya mwaka 2011.
Aidha, anaiomba mahakama itamke kama bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.
Chapisha Maoni