0
Nyota mchezaji wa kimataifa kutoka
Ufaransa, Dimitri Payet amesema kuwa
hakukusudia kumchezea rafu nahodha
wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano
Ronaldo katika fainali za kombe la Euro
2016.
Hii ni baada ya malalamiko na lawama
katika mitandao ya kijami ya wapenzi wa
kandanda ulimwenguni ikiwemo mama
yake Cristiano Ronaldo kulaumu na
kumtupia lawama Dimitri Payet kwa
kitendo cha kumchezea rafu Cristiano
Ronaldo na kusababisha kutomaliza
mchezo na kuondoka uwanjani,
hatimaye mchezaji huyo wa Ufaransa
ameweka wazi tukio hilo na kufahamisha
ya kwamba hakuwa na nia ya
kumchezea rafu Ronaldo ila ilikua ni
katika hali ya kunyang’anya mpira.
Yote hayo aliyazungumza katika
mahojiano na waandishi wa habari wa
kituo cha habari za michezo cha
BeinSport.

Chapisha Maoni

 
Top