0
Mkongwe ambaye ni mwanariadha wa
kimataifa kutoka Jamaika, Usain Bolt
amethibitisha kushiriki katika michuano
ya Olimpiki mjini Rio de Janiero nchini
Brazil.
Mwanariadha huyo matata ni bingwa wa
dunia wa mbio za mita 200 na mita 100,
aliwahi kutangaza kuwa hatojiunga na
timu yake ya taifa ya riadha ya Jamaica
katika michuano ya Olimpiki
itakayofanyika Agosti 5 hadi 21 mjini Rio
de Janiero nchini Brazil kufuatia jeraha
alilopata. Lakini kwa mujibu wa kamati
ya Olimpiki nchini Jamaica imethibitisha
kwamba Usain Bolt ataipeperusha
bendera ya nchi hiyo katika michuano
hiyo baada ya kamati hiyo kutangaza
orodha ya wanariadha 59 watakaoshiriki
michuano hiyo na yeye akiwemo.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top