0

Mchezaji nahodha wa klabu ya Arsenal,
Mikel Arteta ni miongoni mwa wachezaji
wanaotarajiwa kuhama klabu hiyo majira
haya ya joto. Arteta pamoja na kiungo
wa kati mwenzake Tomas Rosicky
wanatarajiwa kuondoka baada ya
mikataba yao kumalizika.
Nyota huyu alijiunga na klabu hiyo
mwaka 2011 na amewachezea mechi
150 na kufunga mabao 17. Naye,
Rosicky, 35, alijiunga na Arsenal mwaka
2006 na alituzwa kwa kuwachezea
Gunners mechi 246 kipindi cha miaka
10 wakati wa mechi yake ya mwisho
dhidi ya Aston Villa. Arteta,
aliyenunuliwa Everton kwa £10m,
alionekana akitokwa na machozi baada
ya mechi hiyo kumalizika.
Kwa upande wake meneja Arsene
Wenger amesema wachezaji hao wawili
walikuwa ni wa kipekee!



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top