0

Kocha Mkuu wa Mwadui FC ya
Shinyanga,Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema
timu yake kufungwa na Toto Africans katika
michezo ya ufunguzi wa msimu mpya huwa ni
baraka.
Julio ametoa kauli hilo baada ya Jana Jumatano
kikosi chake kuanza msimu mpya wa ligi kuu
bara kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 toka
kwa Toto Africans katika mchezo pekee wa ligi
hiyo uliofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba,Mwanza.
Akifanya mahojiano na kipindi cha michezo cha
TBC Taifa,Julio,amesema siku zote Mwadui FC
inapofungwa na Toto Africans katika michezo ya
ufunguzi huwapa mafanikio mwisho wa msimu.
Amesema "Mwaka juzi tulifungwa na Toto
tukiwa daraja la kwanza katika mchezo wa
ufunguzi tukapanda daraja.Mwaka jana
tukafungwa tena na Toto katika ufunguzi
tukafika nusu fainali ya FA Cup,leo (jana)
tumefungwa tena na Toto katika ufunguzi
naamini kuna mafanikio yanakuja mbele yetu".
Wakati huohuo Julio amewataka waamuzi
wanaochezesha michezo ya ligi kuu bara
kufuata sheria 17 za soka na siyo kuonyesha
upendeleo kama ilivyokuwa katika mchezo wa
jana ambapo mwamuzi alionekana
kuwapendelea wenyeji Toto Africans.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top