Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara
amesema siku ya Jumatatu atazungumza na
waandishi wa habari kuzungumzia mambo kadhaa
yaliyotokea kwenye mpambano wa watani wa jadi,
Simba na Yanga .
Akizungumza baada ya mpambano huo jana,
Manara alisema klabu yake imechukizwa na
maamuzi mabovu ya mwamuzi Martin Saanya na
kudai kuwa Yanga ilibebwa kwa 'mbeleko ya
chuma'.
“Hii ni ishara kwamba hatutazuilika na TFF,
referees na mtu yeyote, mwaka huu ni wetu
hakuna mtu wa kutuzuia, tunao uwezo timu yetu
tumeiona”, amesema Manara ambaye alionekana
wazi kuwa na jazba.
“Tunaenda kuangalia marudio, tukiona kwa namna
yeyote ile Yanga walibebwa hatutakubali, safari hii
kuna jambo litatokea zaidi ya mpira, haiwezekani
timu moja ikawa inabebwa kwa mbeleko ya
chuma, Jumatatu nitazungumza na waandishi wa
habari.”
“Klabu ikiona kitu cha tofauti, itachukua hatua za
makusudi. Kwa sababu timu hii inabebwa, ikienda
kwenye mashindano ya Caf raundi ya kwanza nje.”
“Hatuungi mkono vurugu, lakini mechi hii ina-
tension kubwa lazima marefa wajitahidi
kuchezesha kwa haki, hakuna asiyeona kwamba
yule mchezaji aliushika mpira. Hatutaki fujo
unalazimisha watu wafanye fujo.”
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1
Simba ikisawazisha kwenye dakika za majeruhi
kupitia mpira wa kona wa Shiza Kichuya.
Hata hivyo mashabiki wa Simba walifanya uharibifu
kwa kun'goa viti uwanjani baada ya bao la Amisi
Tambwe anayedaiwa kuushika mpira kabla ya
kufunga, kukubaliwa na mwamuzi.
Kwa maoni yangu viongozi wa Simba wanapaswa
kukemea utovu wa nidhamu ulioonyeshwa na
mashabiki wake.
Haikuwa sahihi kufanya uharibifu wa miundombinu
ya uwanja kwa namna yoyote hata kama
walichukizwa kwa kiasi chochote.
Timu zetu zitapata wakati mgumu pale
zitakaposhiriki michuano ya Kimataifa kama tabia
hii itaachwa iendelee.
Ni hivi majuzi tu tumeshuhudia timu ya ES Setif ya
Algeria ikiondoshwa kwenye michuano ya klabu
bingwa barani Afrika baada ya mashabiki wake
kufanya vurugu kwenye moja ya michezo yake.
Shirikisho la soka duniani, FIFA limekuwa
likikemea vurugu kwenye mchezo wa mpira wa
miguu, soka ni mchezo wa kiungwana.
Ni dhahiri Simba itawajibika kukarabati uharibifu
uliofanywa na mashabiki wake na huenda ikajikuta
matatizoni kwa kulipishwa faini.
Aidha TFF nayo inapaswa kuwa makini na aina ya
waamuzi inaowatumia kuchezesha mchezo wa
Simba na Yanga kwa kuwa inafahamika mchezo
huo huwa na ushindani wa aina yake kutokana na
historia ya klabu hizo.
TFF inapaswa kujiridhisha wa maamuzi
yaliyofanyika na kama itaona waamuzi
hawakutenda haki kwa makusudi maeneo kadhaa
basi wachukuliwe hatua za kinidhamu ili kuondoa
nadharia ya kuwa huenda nao wanahusika
kuzibeba baadhi ya timu.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.