Mchezo huo licha ya kuisha kwa sare ya
kufungana 1-1, lakini uligubikwa na vurugu
kubwa hasa baada ya Yanga kupata bao la
kwanza lililofungwa na Amisi Tambwe
Kufuatia vurugu zilizozuka jana uwanja wa taifa
Dar ea Salaam kwenye pambano la Dar Derby
kati ya Yanga na Simba Waziri wa michezo Nape
Nnauye amezipiga marukufuku klabu hizo
kongwe kuutumia uwanja huo katika mechi zao
za ligi ya Vodacom inayoendelea.
Waziri Nape ameiambia chanzo cha habari hii Goal na Africa Newss Sports , kwamba hawato
zipa klabu hizo mapato ambayo yamekusanywa
kwenye mchezo huo na badaya yake watatumia
pesa hizo kwa ajili ya kukarabati miundombinu
ya uwanja huo ambayo imeharibiwa na
mashabiki wa pande zote mbili.
“Kama Serikali hatuwezi kuvumilia upuuzi huu
nivyema tukawapa nafasi watu wengine
wastaarabu ambao wanaweza kuutumia uwanja
huu na siyo Simba na Yanga ambao wamevunja
mageti manne mawili upande wa Yanga na mawili
mengine upande wa Simba lakini pia viti
vipatavyo 1,781 vimengolewa na mashabiki wa
Simba,”amesema Waziri Nape.
Mchezo huo licha ya kuisha kwa sare ya
kufungana 1-1, lakini uligubikwa na vurugu
kubwa hasa baada ya Yanga kupata bao la
kwanza lililofungwa na Amisi Tambwe ambaye
inadaiwa kabla ya kufunga bao hilo aliushika
mpira.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.