0

Muingereza huyo amepata kibali machoni pa Mourinho wake, ambaye hivi karibuni amedai kuwa Rashford ni moja ya wachezaji anaowaamini sana
Mshambulizi wa Manchester United Marcus Rashford amedai kuwa ameweza kumshawishi Jose Mourinho kumpatia nafasi kwa kujituma zaidi.
Mchezaji huyo kinda wa miaka 19 amekuwa na msimu murua kwa mara nyingine baada ya kufunga mabao 11 na kutengeneza mabao
matatu katika michuano yote msimu huu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amepata kibali machoni pa meneja wake, ambaye
hivi karibuni amedai kuwa Rashford ni moja ya wachezaji anaowaamini sana kwenye kikosi chake.
"Ni jambo kubwa meneja kama yeye anaposema hivyo," Rashford alikiambia Premier League
Productions. "Jambo jema ni pale unapopata fursa ya kucheza. Hakusema tu 'naam, sasa upo
vizuri cheza kila mechi'. Ametufanya sote tujitume ili kuweza kumshawishi na kupata
heshima yake.
"Wakati mwingine ni vigumu na wakati mwingine ni rahisi lakini wachezaji wanapambana kuimarika
kufanya kazi na kocha wetu. Inavutia kuona kila mtu amefenya jitihada mwaka huu."
Kutokana na Zlatan Ibrahimovic kukosekana kwa sababu ya majeraha, Rashford anaweza kuanza
mechi ya Jumatano ijayo fainali ya Europa dhidi ya Ajax mjini Stockholm.


Chapisha Maoni

 
Top