0
Mshambulizi wa Liverpool Divock
Origi ametaja ushindi wao wa Jumapili
14 Mei dhidi ya Westham United kuwa
hatua muhimu kuelekea wao kutinga
michezo ya ligi ya Kuu ya Mabingwa
barani Ulaya kwa msimu ujao.
Akizungumza na BBC Swahili baada
ya kuchangia ushindi wa 4-1 kwa bao
moja, Origi, mwenye umri wa miaka
22, ambaye ana uwezo wa
kuzungumza lugha ya Kiingereza na
Kifaransa, aliwaacha wengi vinywa
wazi huku akitupia Kiswahili katika
mahojiano hayo ya moja kwa moja.
Tunafurahi
- Ilikuwa game ngumu lakini
tulionyesha offensive qualities zetu.
Tunafurahi sana ilkuwa game very
important for us so in the end its
three points, tumefurahi.
Kwanza tunajua Arsenal wana a lot of
qualities so .. ilibidi tufocus on our
game in end tunafurahi sana.
Ushindi huo umeiweka Liverpool
katika nafasi bora ya
kushiriki michuano hiyo ambayo Origi
anaamini kuwa ni muhimu kwa
miamba haso wa Uingerreza.
- Of course champions League ni
muhimu sana kwa sisi sote, alisema
Divock.
Familia
 Mzaliwa huyo wa Ostend Ubelgiji, ana
asili yake nchini Kenya anakotoke
babake na mshambulizi za zamani wa
Harambee Stars, Mike Okoth.
Vijana wa Jurgen Klopp wanahitaji
ushindi wowote katika mechi yao ya
mwisho dhidi ya Middesbrough,
ambayo tayari umeshushwa daraja, ili
kujikatia ticketi ya michuano ya hio ya
Ulaya.

Chapisha Maoni

 
Top