0
Kocha wa Kihisipania Pep Guardiola anaamini James Rodriguez anaweza kufanikiwa zaidi Ligi Kuu Uingereza endapo atatua Manchester Bosi wa Manchester United Pep Guardiola
amebashiri kuwa James Rodriguez atafanikiwa kwenye Ligi Kuu Uingereza ikiwa ataondoka Real
Madrid kujiunga na Manchester United.
Habari zinadai kuwa James Rodriguez
ameruhusiwa kutua United baada ya habari mchanganyiko kutoka Hispania ambako amekuwa akitumiwa na Zidane kutokea benchi.
City hawamo kwenye mbio za kumwania
mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia lakini alipoulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi dhidi ya West Bromwich
Albion, Guardiola alisme kwamba mchezaji huyo hatapata tabu kulizoea soka la Uingereza. Kocha huyo wa zamani wa Barcelona aliwaambia
waandishi: "Kwa maana ya ubora, hakuna shaka juu yake katika Real Madrid, kwa sababu wachezaji wenzake katika kikosi hicho ni bora
zaidi.
"Wachezaji wote bora duniani wanaweza kucheza ligi zote, itategemeana na timu na wachezaji wenzake, lakini ubora wake ni thabiti." Rodriguez ameanza mechi 13 tu La Liga msimu huu, na nyingine nne katika Ligi ya Mabingwa.

Chapisha Maoni

 
Top