wa Mara, na aliyewahi kugombea
Urais ndani ya Klabu ya Simba
Michael Richard Wambura
ameshindwa kutaja waziwazi kama
atagombea nafasi yoyote kwenye
uchaguzi Mkuu Wa Shirikisho la Soka
nchini TFF.
Akizungumza kwenye Kipindi cha
Michezo kinachoendeshwa na Radio
Free Africa, Wambura amesema hata
yeye Bado hajui kama atawania nafasi
yoyote Lakini muda ukifika Atatangaza
nafasi atakayowania ili kukuza soka
hapa nchini.
-Katika Mpira nimekuwapo kwa muda
mrefu Sana, na suala la uongozi ni
demokrasia Kila mtu anaruhusiwa
kusaidia pale anapoweza, kwa sasa
Mimi ni Mwenyekiti wa mkoa wa Mara
na bado najaribu kuangalia navyoweza
kuisaidia soka La mkoa Wangu, Ila
Kamati ya uchaguzi ya TFF ikitangaza
mchakato nitatangaza Rasmi wapi
nitaingiza Miguu yangu" Alisema.
Jamal Malinzi.
Kuhusiana na uongozi wa Sasa
Wambura amesema japokuwa
unamakosa Mengi Lakini kuna Mengi
pia ambayo wamesaidia kuinuka kwa
soka na kwa hilo hatosita kutoa
pongezi kwa Jamal Malinzi.
-Labda Niseme kitu kimoja, uongozi
wa Mpira wa Miguu ni mgumu Sana,
ni rahisi sana kulaumiwa na rahisi
sana kupongezwa na Kwetu hapa
Tanzania bado Yupo nyuma mno, Ila
uongozi uliopo madarakani umefanya
kazi yao" Wambura aliongeza.
TFF Wanatarajia kufanya uchaguzi
Mkuu wa Viongozi Agosti 12 Mwaka
huu, Huku bado kukiwa na usiri kwa
wale ambao wanataka kugombea
nafasi hizo

Chapisha Maoni