0
Jumla ya wachezaji Watano
wamechaguliwa kuwania tuzo ya
Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara Kwa msimu
wa Mwaka 2016/17.
Wachezaji hao ni Haruna Niyonzima
na Simon Msuva wa Timu ya Yanga
SC, Aishi Manula WA Azam FC, Shiza
Kichuya, na Mohamedi Hussein Wote
wa Timu ya Simba SC.
Wachezaji hawa watapigiwa kura na
makocha wakuu , makocha wasaidizi
na manahodha wa vikosi vya ligi kuu
Tanzania bara, Sambamba na hao pia
wahariri kutoka vyombo mbalimbali
vya michezo nchini.
Upigaji Kura.
Zoezi linaanza rasmi Mei 18 na
mwisho wa kupiga kura ni saa sita
kamili usiku wa tarehe 23 Mei 2017.
Hafla ya utoaji tuzo hizo zitafanyika
Mlimani City tarehe 24 Mei 2017 na
zoezi zima kuratibiwa na kamati ya
ushauri ya raisi wa Shirikisho la soka
Tanzania 'TFF'.

Chapisha Maoni

 
Top