Klabu ya Azam FC imefanikiwa kupata saini ya Mshambuliaji wa Timu ya Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ambaye amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili. Milioni 40
Aidha Azam wamewapiku Yanga kusaini mchezaji huyo ambaye wamekuwa wakimwinda kwa muda baada ya Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara kushindwa kumshawishi Mbaraka kutia saini Wino.
Yanga walikuwa wametoa dau la milioni 50 huku Azam wakitoa milioni 40 kwa maana ya milioni 20 kila mwaka.
Mshambuliaji wa pili
Mbaraka ambaye aliwahi kuitimikia timu ya Simba alipata mafanikio makubwa msimu uliopita akiichezea Kagera Sugar na kufanikiwa kufunga mabao 12 pamoja na kutwaa taji la mchezji bora chipukizi Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
Mbaraka anakuwa Mshambuliaji wa pili kusainiwa na Azam Fc ambao pia wamemsaini Mshambuliaji Waziri Junior akitokea Timu ya Toto Africans ya kutoka Jijini Mwanza.
Chapisha Maoni