0
Uongozi wa Klabu ya Mbeya City umetolea ufafanuzi sababu za kuwasusa wachezaji wao Watatu raia wa Uganda kwa Zaidi ya Miezi miwili hali iliyofanya kushindwa kujihudimia na Kukimbilia kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya kuomba Msaada.
Akithibitisha Taarifa za kuwatelekeza wachezaji hao Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Emanuel Kimbe amesema wachezaji hao awali walivunja kipengele cha mkataba wao ambao ulikuwa ni mkataba wa muda wa miezi mitano, na wakijua wazi kuwa wapo katika kipindi cha uangalizi waligoma kuambatana na Timu kwa Kambi ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
-Wale walijitoa kwenye Timu hata kabla ya Mechi na Yanga, kwa sababu kabla ya Kwenda Dar timu ilienda Sumbawanga kwa Kambi fupi sasa wao waligoma kwenda huko kwa sababu zao wenyewe ambazo kimsingi hazikuwa na mashiko yoyote, sasa walipojitoa kwenye Timu inaamana timu haihusiki na wewe tena,” Alisema.
Aliongeza kuwa ‘Kwanza walikuwepo kwenye kipindi cha Probation (Uangalizi) ili waweze kusajiliwa rasmi kwani hawakuwa wamesajiliwa kwa kipindi chote hicho, kwa kuwa walikuwa na mikataba ya Muda ya Miezi mitano, sasa walipokataa kwenda Sumbawanga moja ya vigezo walikosa kwa sababu huwezi kuwa kwenya probation halafu ukachagua kazi ya kufanya kwamba hii nafanya hii siifanyi”.
Ila Tutalishughulikia.
Kimbe amesema kwa kuwa wamekwenda kwa Mkuu wa Mkoa na tayari wameagizwa kulishughulikia suala hilo basi kama Uongozi wa Klabu wanaahidi kulishughulikia, hata hivyo wamesema hawakujua kama kuna wachezaji wamebaki Mbeya kwani tayari wachezaji wote wamekwishaondoka kasoro wao.
Mzizi wa Tatizo.
Ikumbukwe kwamba Ijumaa Wachezaji watatu wa Mbeya City Mshambuliaji Tito Okello, Beki Wiliam Otongo na Winga Mayanja Hood walifika katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya  Amosi Makala wakidai kuwa Wanadaiwa zaidi ya Shilingi Millioni 12.2 kama deni la Chakula baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Mbeya City kwa zaidi ya Miezi Miwili sasa.
Wachezaji hao wamesema madeni hayo yametokana na kutolipwa fedha zao za mshahara na chakula kwa miezi miwili, kama mkataba ambao waliingia na Klabu hiyo Desemba Mwaka jana ulivyoeleza, walidai pia wameshinda Njaa kwa Zaidi ya siku tatu kwa kuwa Hotel waliyokuwa wanakula imegoma kuwapa chakula kwa kuwa na Madeni Mengi.

Chapisha Maoni

 
Top