Jeshi la Polisi lasema, Vijana 17 waliokamatwa jijini Arusha si Al shabaab bali ni watuhumiwa waliohusika na tukio la ulipuaji wa bomu
JESHI la Polisi nchini limekanusha kwamba
watuhumiwa 14 waliokamatwa na kufikishwa
mahakamani mkoani Arusha hawahusiki na
kundi la Al-Shabaab kama ilivyoripotiwa na
baadhi ya vyombo vya habari hapo jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam jana, Mkurugezi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu, alisema
waliokamatwa ni watuhumiwa waliohusika na
tukio la ulipuaji wa bomu katika baa ya Night
Park na bomu lililotegwa katika baa ya
Washington Aprili 13 mwaka huu jijini Arusha.
Chapisha Maoni