0
NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry 'Monalisa' , George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari eneo la Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye blog yake kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hiyo huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka waanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini. Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae leo asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza. Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hiki ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka. Batuli: - Niongee nini, niseme nini Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng, R.I.P My brother, My shemeji, My director......Eeeeeh Mola mpokee George Tyson wetu, Poleni wasanii wenzangu, Poleni team nzima ya the mboni show thembonishow Pole Monalisa wangu Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA kusema ila asante baba wa mbinguni kwa kila jambo. ...mola mpokee ndugu yetu, kwa mikono salama na umlaze pema peponi ameen.....R.I.P George Tyson. Agness Masogange: R.I.P George tyson mm siamin bado jmn E Mungu tuhurumie waja wako! Flaviana Matata : This is very sad aisee,Rest In Peace Tyson.Mungu kakupenda zaidi, - monalisa pole sana dadangu,Mwenyezi Mungu awatie nguvu Wema Sepetu - Kwa mara ya tatu bila hata kupumzika week... tunamzika mwenzetu mwingine... George Tyson.... Dah... Im just speechless.. RIP brother... Dah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee.... Pole dada akee ... Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya @thembonishow .... Pigo kubwa tena kwa wasanii.... Tunaisha tu jamani. Aunty Ezekiel - Mungu wang Naomba useme na sisi jaman Mungu baba tuone sisi jaman Naumia siwezi elezea jaman RIP Tyson wang jaman Rip director .....Nakosa lakusema

Chapisha Maoni

 
Top