Wagonjwa wapya 21 wa Dengue wagundulika.....Hii inafanya idadi ya wagonjwa hao kufikia 926 tangu ugonjwa huo ulipoanza mwaka huu
Ugonjwa wa homa ya dengue umeendelea
kuwasumbua wakazi wa Dar es Salaam,
ambapo wagonjwa wengine 21 waligundulika
kupatwa na ugonjwa huo.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Ufuatiliaji wa
Magonjwa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alex
Mkamba, ilisema Hospitali ya Temeke ina
wagonjwa 13, Kinondoni watatu na Ilala
wanne.
“Kati ya wagonjwa hao 21 ni mmoja tu
aliyepata matibabu na kuruhusiwa lakini
wengine 20 wameendelea kulazwa kutokana na
hali zao,” alisema Mkamba.
Aidha, alisema mapambano dhidi ya ugonjwa
wa dengue, si ya Serikali peke yake, bali
wananchi wote na kutaka ushirikiano zaidi
kutokomeza mazalia ya mbu na kuweka
mazingira katika hali ya usafi kuzuia mbu
kuzaliana. Alisema mbali na Serikali kupuliza dawa katika
kata 78 jijini humo, kuliko na idadi kubwa ya
waathirika wa ugonjwa huo, mabasi yaendayo
mikoani yanaendelea kupuliziwa dawa ya kuua
mbu, kuhakikisha mbu hawasafiri kuenea zaidi
nchini.
Taarifa ya juzi inaonesha kuwa Hospitali ya
Temeke ilipokea wagonjwa wanane, Ilala
wagonjwa 11, Kinondoni wagonjwa 17, Sinza
mgonjwa mmoja na Kinondoni kwa Dk Mvungi
mgonjwa mmoja.
Mpaka sasa watu 926 wameugua ugonjwa huo
tangu ulipoanza mwaka huu.
Chapisha Maoni