Ray C sasa ahitaji mpenzi Ya wazee....Asema Mapenzi ya vijana yamempa majuto ya milele
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Rehema
Chalamila ‘Ray C’, amesema kwa sasa hana
mpango wa kuwa na mahusiano ya kimapenzi
na mtu, na kama ikitokea basi atamtaka kuwa
na miaka kuanzia 60.
Akizungumza katika kipindi cha ‘The Sporah
Show’, Ray C alisema anahitaji wanaume wa
umri mkubwa, kwa kuwa wanajua
wanachokifanya, na kukiri kwamba vijana
walichangia katika kurudisha nyuma maisha
yake.
Msanii huyo ambaye kwa sasa ameanzisha
asasi yake ya kupambana na dawa za kulevya,
kutokana na yeye kuwa mmoja wa waathirika
wa dawa hizo, alisema katika moja ya mambo
anayoyajutia ni kuwa na mahusiano na vijana,
jambo ambalo hataki kukumbuka
walichomfanyia hadi kudhalilika mbele ya
jamii.
Hata hivyo, alitumia fursa hiyo kuwaasa
wazazi kutowatenga watoto wao ambao
wamejidumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za
kulevya na badala yake, wawakumbatie na
kuwaonyesha njia kama mama yake
alivyofanya na kurudia hali yake ya kawaida.
Kuhusu kurudi kwenye muziki, Ray C alisema
yupo mbioni na tayari ameshatengeneza
nyimbo kadhaa, ambapo hivi sasa atakuwa
akiimba miondoko tofauti tofauti, ikiwemo
taarabu.
Katika kurudi kwenye muziki, jambo la kwanza
alisema anatarajia kupunguza mwili wake kwa
kufanya mazoezi, kwani hata daktari wake
alishamwambia anatakiwa kupungua kutokana
na umri wake kutoendana na kilo alizonazo.
Alipoulizwa mwanamuziki ambaye kwa sasa
anamkubali Bongo, Ray C alisema wa kwanza
ni AT akifuatiwa na Recho kutoka Jumba la
Kukuza Vipaji (THT).
Chapisha Maoni