0
LIVERPOOL imerudi vizuri katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya, baada ya usiku huu kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Ludogorets Uwanja Anfield.

Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli
amefunga bao lake la kwanza leo Liverpool dakika ya 81, kabla ya Dani Abalo kuisawazishia Ludogorets.
Nahodha Steven Gerrard aliihakikishia
Liverpool kushinda mechi ya kwanza ya
makundi kwa bao la penalti dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet,
Manquillo, Lovren, Sakho, Moreno,
Henderson, Gerrard, Lallana/Borini dk67,
Sterling, Coutinho/Lucas dk67 na Balotelli. Ludogorets: Borjan, Caicara, Moti, A Aleksandrov, Minev, Dyakov, Abel, M Aleksandrov, Marcelinho, Misidjan na Bezjak.

Chapisha Maoni

 
Top