
Marek Suchy alijifunga dakika ya 14 kuipa Real bao la kuongoza kabla ya Gareth Bale kufunga la pili akimalizia pasi ya Luka Modric dakika ya 30.
Bale akamtilia krosi maridadi Cristiano
Ronaldo kuifungia Real bao la tatu dakika ya 31 kabla ya James Rodriguez kufunga la nne dakika ya 36 na Derlis Gonzalez kuifungia Basle bao la kufutia machozi dakika ya 37.
Karim Benzema alihitimisha shangwe za
mabao za Real Madrid kwa bao la tano dakika ya 79. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Nacho, Kroos, Rodriguez, Bale, Modric, Ronaldo na
Benzema.
Basle: Vaclik, Samuel, Schar, Suchy, Safari, Zuffi, Frei, El-Nenny, Xhaka, Streller na Gonzalez.
Chapisha Maoni