0
BAO la dakika ya 83 la Martin Demichelis
limeinusuru Manchester City kulala mbele ya Arsenal baada ya kupata sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.

Sergio Aguero alitangulia kuifungia City
dakika ya 28 akimalizia kazi nzuri ya Jesus Navas kabla ya Jack Wilshere kuisawazishia

Arsenal kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Aaron Ramsey

Alexis Sanchez akaifungia Arsenal bao la pili dakika ya 74 kabla ya Debuchy kuisawaishia City. Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck alikaribia kufunga dakika ya 11 baada ya kugongesha mwamba, wakati
kiungo mpya wa Man City, Frank Lampard alionyeshwa kadi ya njano.

Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny,
Debuchy/Chambers dk81, Mertesacker,
Koscielny, Monreal, Flamini/Arteta dk95,
Wilshere, Ramsey, Alexis, Ozil na Welbeck/ Oxlade-Chamberlain dk88.

Man City: Hart, Zabaleta, Kompany,
Demichelis, Clichy, Fernandinho/Kolarov
dk77, Lampard/Nasri dk45, Navas, Silva,
Milner, Aguero/Dzeko dk67.

Chapisha Maoni

 
Top