0
ATLETICO Madrid imeendeleza ubabe wake kwa Real Madrid baada ya kuichapa mabao 2-1 usiku huu Uwanja wa Bernabeu mjini Madrid, Hispania katika mchezo wa La Liga.
Atletico Madrid ilipata bao la kuongoza dakika ya 10 tu kupitia kwa Tiago kabla ya Real Madrid kusawazisha dakika 16 baadaye kupitia kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa penalti.

Arda Turan aliifungia bao la ushindi Atletico dakika ya 76 akimalizia kazi nzuri ya Raul Garcia. Kocha Diego Simeone alitazama mchezo huo kutokea jukwaani kutokana na
kuwa anatumia adhabu.


Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Atletico kuwafunga mfululizo majirani zao hao wa Madrid.

Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa/Varane dk78, Pepe, Ramos, Coentrao, Modric, Kroos, Bale/Isco dk72, Rodriguez, Ronaldo, Benzema/Hernandez dk63.

Atletico Madrid: Angel Moya, Juanfran,
Miranda, Godin, Siqueira, Garcia, Gabi/Turan dk60, Tiago, Koke, Jimenez/Griezmann dk64, Mandzukic/Suarez dk78.

Chapisha Maoni

 
Top