0
BAO pekee la Gabby Agbonlahor dakika ya tisa siku tatu tangu asaini Mkataba mpya wa miaka minne, limeipa Aston Villa ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Liverpool Uwanja wa
Anfield jioni ya leo.

Hicho kinakuwa kipigo cha pili msimu huu kwa Liverpool, baada ya awali kufungwa mabao 3-1 na Manchester City Uwanja wa Etihad.

Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli
aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan, alichezea kwa mara ya kwanza Liverpool lakini hakuweza kuiepusha na kipigo hicho.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet,
Manquillo, Lovren, Sakho, Moreno, Gerrard, Henderson, Markovic/Borini dk71, Coutinho, Lallana/Sterling dk61 na Balotelli/Lambert dk71.

Aston Villa: Guzan, Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Cleverley/Sanchez dk86,رWestwood, Delph, Agbonlahor/Bent dk90, Weimann/N'Zogbia dk72 na Richardson.

Chapisha Maoni

 
Top