(CHADEMA), mkoani Simiyu, kimeendelea na msimamo wa kufanya maandamano ambayo yamepangwa kufanyika leo wakipinga kuendelea
kwa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Mshuda Wilson, alisema maandamano hayo yatakuwa ya amani akilitaka Jeshi la Polisi kutotumia nguvu ili kuyazuia kwani ni haki yao
kikatiba kufanya maandamano.
Alisema maandamano hayo yataanza saa tatu asubuhi yakishirikisha wanachama wa CHADEMA mkoani humo na tayari wamelitaarifu jeshi hilo
ambalo limeyapinga, lakini watayafanya.
"Maandamano haya yatapita barabara ya Somanda, Malambo, Sima hadi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa...tutakuwa na mabango yanayopinga kuendelea kwa Bunge la Katiba hadi
Oktoba 4 mwaka huu," alisema.
Katika hatua nyingine, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani humo, Venance Kimario, alisema jeshi hilo limeyazuia maandamano hayo na kuyapiga
marufuku.
Alisema viongozi wa chama hicho walipeleka barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamano, lakini walikataa na kuwataka wayasitishe kwani
hayapo kisheria.
"Tumejipanga kupambana na mtu au kikundi cha watu ambao watakiuka amri au maelekezo halali ya polisi pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria.
"Tunawaomba wanachama na viongozi wa CHADEMA, waache kuratibu maandamano hayo, wananchi endeleeni na shughuli zenu kwani maandamano hayako kisheria, tutapambana nao,"
alisema.
Polisi wauteka Mji wa Bariadi
Katika hali isiyo ya kawaida, askari polisi wakiwa katika magari mawili, juzi na jana wamekuwa wakizunguka kwenye mitaa mbalimbali ya Mji wa
Bariadi ili kuzuia maandamano hayo kama yatafanyika.
Hali imesababisha hofu kwa wananchi mjini humo kwani si kawaida ya jeshi hilo kufanya doria kama hiyo huku wakiwa na rungu, fimbo pamoja na
mabomu ya machozi.
Askari hao wameonekana wakizunguka Ofisi ya CHADEMA wilayani humo ambako kuna mitaa yenye maduka mengi na njia zote ambazo zimetajwa kuhusika na maandamano.
Chapisha Maoni