0

Majeshi ya Marekani yameanza rasmi
mashambulizi ya anga nchini Syria yakilenga kundi la kigaidi la ISIS (Islamic State of Iraq and Syria).

Makao Makuu ya Ulinzi ya Marekani yameeleza kuwa wanafanya mashambulizi ya mchanganyiko
kwa kutumia mabomu, wapiganaji wa ardhini pamoja na majeshi ya Anga kutoka nchi za Mashariki ya Kati zinazowaunga mkono.

Lakini habari za mashambulizi yaliyoanza zilitolewa na raia wa Syria aliyetweet kuhusu kile anachokisikia katika mji aliopo wa Raqqa ambako
kuna makao makuu ya kundi hilo.

Mtu huyo anaetumia jina la Abdulkader Hariri aliandika kuwa milipuko mikubwa imelenga makao makuu ya ISIS na kwamba anga lote limejaa ndege za kivita na drones.

Baadae Agency ya wanaharakati nchini Syri ilipost video fupi inayoonesha kwa mbali mashambulizi ya Marekani.

Chapisha Maoni

 
Top