0
KIPA bwana mdogo wa Chelsea Thibaut
Courtois ambaye kwasasa ndiye chaguo la kwanza la kocha Jose Mourinho, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.

Hatua hiyo inazidi kumweka pabaya kipa Petr Cech ambaye kwa miaka kumi iliyopita alikuwa kipa namba moja.
Courtois ameanza kuichezea Chelsea msimu huu licha ya kusajiliwa tangu mwaka 2011 ambapo alilazimika kupelekwa Atletico Madrid kwa
mkopo ili kuongeza uzoefu.

Courtois akaicheza kwa mafanikio Atletico Madrid kwa misimu mitatu mfululizo baada ya kujiunga na Chelsea kutoka Genk ya nyumbani
kwao Ubelgiji.

Akarejea Stamford Bridge msimu huu na
kucheza mechi yake ya kwanza dhidi Burnley na kuisadia Chelsea kuibuka na ushindi wa 3-1 na baada ya hapo akamsugulisha benchi Petr Cech
mechi zote zilizofuata.

Sasa Cech, 32 atalazimika kuangalia
uwezekano wa kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine pindi utakapowadia msimu wa usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.
Taarifa iliyotolewa kupitia mtandao rasmi wa Chelsea imesema: “Chelsea Football Club ina furaha kutangaza kuwa Thibaut Courtois, 22 amesaini mkataba mpya wa miaka mitano.”

Chapisha Maoni

 
Top