0
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu
kimedai kuwa Bunge Maalumu la Katiba
linaloendelea linaendeshwa kimabavu kwa kutumia fedha za wananchi bure wakati wakijua fika hakuna katiba
itakayopatikana.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadam (LHRC) Dk. Helen Kijo- Bisimba, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni gogota) kwa wananchi.

"Cha kusikitisha ni kwamba tumepoteza
mabilioni ya fedha ambazo zingeweza
kusaidia kwenye sekta mbali mbali
zikiwemo za afya na elimu kwa kuwalipa
wajumbe wa bunge la katiba," alisema.

Alisema wakati wa kampeni hiyo ambayo imefanyika kwenye mikoa 20 nchini kituo hicho kimebaini kuwa wapo asilimia kubwa ya wananchi wanakerwa na mwenendo wa mchakato wa bunge hilo kwa kuchakachua maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya
mabadiliko ya katiba.

Alisema wakati wa kampeni hiyo ya gogota kituo hicho kimefanikiwa kufika kwenye wilaya zote, na kata tatu kwa kila mkoa ambapo kilifanikiwa kurudisha ajenda ya katiba na uelewa wa rasimu ya pili ya katiba kwa wananchi.

Alisema hiyo ni moja ya mafanikio
waliyoyapata kuyajua kwa wananchi
kwenye kampeni hiyo ambayo ililenga
kuhamasisha wananchi kushiriki katika
mchakato hususani kufuatilia bunge la
katiba na upigaji wa kura ya maoni muda utakapo fika.

Pamoja na mafanikio hayo pia kitu hicho
kimekutana na changamoto mbali mbali
ikiwemo ya uelewa mdogo kuhusu katiba hususani walio pembezoni mwa miji.

Alitaja mikoa hiyo ni Arusha, Tanga,
Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mbeya,
Rukwa, Kilimanjaro, Manyara, Katavi,
Iringa, Mara, Njombe, Ruvuma, Pemba
Kaskazini, Kusini, Pemba mjini Magharibi, Unguja Kusini na Kasazini.

Alitaja changamoto nyingine ni kutokujua kusoma na kuandika kwa baadhi ya wananchi, umangi meza kwa badhi ya viongozi wa mikoa, hofu ya kutopata katiba na mfumo dume kwenye jamii.

Chapisha Maoni

 
Top